Saturday 31 July 2010

Mapishi ya Vitumbua



Baada ya kumiss vitafunio vya nyumbani nikaamuua kupika vitumbua.

Recipe ya vitumbua vyangu nikama ifuatavyo:

  • Unga wa mchele ( Vikombe 2 vikubwa)
  • Sukari (Nusu ya kikombe kikubwa)
  • Hamira ( Nusu ya kijiko cha chai)
  • Hiliki (Nusu ya kijiko cha chai)
  • Tui la nazi ( Kikombe kimoja kikubwa)
  • Unga wa ngano (Vijiko viwili vya chakula)
  • Mafuta ya kuchomea (Vegetable oil)
Matayarisho

Unachanga unga, sukari, hamira, hiliki, unga wa ngano na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastiki. Kisha unaukoroga mpaka mchanganyiko unakuwa kama uji mzito. Kava bakuli lililokuwa na mchanganyiko kisha hifadhi katika sehemu yenye joto kwa muda wa masaa matatu. 

Jinsi ya kupika

Weka chuma cha kuchomea vitumbua katika moto wa wastani, kisha weka mafuta kwenye chuma cha kuchomea ( Kijiko kimoja cha chai) mafuta yakisha pata moto tia uji wako (upawa mmoja) katika kila shimo la chuma cha kuchomea. Acha mpaka kitumbua kikauke kisha geuza na tia mafuta. Acha upande wa pili wa kitumbua mpaka uwe rangi ya kahawia na hapo kitumbua kitakuwa kimeiva utakitoa. Rudia hatua hizo kwa vitumbua  vyote vilivyobaki.

4 comments:

  1. Asha wewe ndio umefanya blog ya maana. Keep up the good work. Asante sana kwa kutupatia mapishi mbalimbali.
    pat

    ReplyDelete
  2. this is nice a lovely idea.Yaani umefanya kitu cha maana sana kufungua hii blog.maana wengne hatujui kupika sasa kupika tutajua kupitia hapa.asante sana,keep it up!!

    ReplyDelete
  3. Hongera sana kwa uamuzi wenye busara kauanzisha blog hii.Kupitia humu nimejivunza mapishi mapya na kuboresha ninayoyajua.Keep it up and be blessed!

    ReplyDelete
  4. Asante sana wadu wote hapo juu, mnakaribishwa sana na tushirikiane.

    ReplyDelete